Connect with us

News

VIDEO: Kenyatta atangaza kufungwa kwa shughuli katika Kaunti 5 kukabiliana na Covid-19

Published

on

NA BMJ MURIITHI

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Ijumaa alitangaza masharti makali katika juhudi za serikali yake kukabiliana na kuenea kwa kasi kwa maambukizi ya virusi vya Corona.

Kwenye hotuba aliyoitoa muda mfupi baada ya saa tisa alasiri kutoka Ikulu mjini Nairobi, Kenyatta alisema wimbi la tatu la ugonjwa wa Covid-19 limesababisha hali ya wasiwasi na sintofahamu kwa sababu ya ongezeko kubwa la maambukizi ndani ya kipindi cha siku chache.

“Nairobi, Kajiado, Machakos, Kiambu na Nakuru ndizo kaunti zilizoathiriwa zaidi,” alisema Kenyatta.

Aliongeza kuwa kwa kila watu mia moja waliopimwa, 22 walipatikana na virusi hivyo.

“Hali hii inasababisha changamoto kwa mfumo wa afya,” alisema.

Haya yanajiri huku vifo vinavyotokana na ugonjwa huo vikiripotiwa kuongezeka kila uchao katika sehemu mbalimbali za taifa hilo la Afrika Mashariki.

“Kwa sababu hizo, baada ya kushauriana na wataalam, baraza la kitaifa la kupambana na virusi vya Corona na  magavana, natangaza amri ya kiutendaji namba 2 ya mwaka wa 2021,” alisema Kenyatta, ambaye wiki mbili zilizopita alikuwa ametangaza masharti mapya ya kukabiliana na ongezeko la maambukizi ambalo lilikuwa limeshuhudiwa hapo awali.

Kwenye hotuba yake ya Ijumaa, Rais Kenyatta alitangaza hatua zifuatazo:

  1. Marufuku ya safari za barabara, reli na angani ndani na nje ya kaunti za Nairobi, Kajiado, Machakos, Kiambu na Nakuru hadi hapo itakapotangazwa tena. Hata hivyo alisema safari za kimataifa zitaendelea ila kwa kuzingatia kanuni zilizowekwa.

 

  1. Hakuna mikutano ya aina yoyote katika kaunti za Nairobi, Machakos, Kajiado, Kiambu na Nakuru hadi hapo itakapotangazwa tena.

 

  1. Bunge la kitaifa, la seneti na yale ya kaunti hizo nne yametakiwa kwenda mapumzikoni hadi itakapotangazwa.
READ ALSO  "It was all God’s doing" Ivy Chelimo responds after being invited to dinner by the DP

 

  1. Amri ya kutotoka nje kuanza saa mbili usiku na kumalizika saa kumi asubuhi katika kaunti za Nairobi, Nakuru, Machakos, Kiambu na Kajiado, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo ilikuwa inaanza kutekelezwa saa nne usiku.

 

Katika kaunti zingine amri ya kutotoka nje itaendelea kama ilivyo sasa, kuanzia saa nne usiku hadi kumi asubuhi.

 

  1. Serikali imefuta vibali vyote maalum vya kuwaruhusu baadhi ya watu wanaotoa huduma muhimu kutoka na kuingia kwenye kaunti hizo hadi uhakiki wa Wizara ya Mambo ya Ndani ufanyike.

 

  1. Kushiriki ibada kwa kuhudhuria binafsi katika Nairobi, Nakuru, Machakos, Kiambu, na Kajiado kumesitishwa hadi pale itakapotangazwa tena.

Kaunti zingine zinaruhusiwa kwendelea na ibada za kuhudhuria moja kwa moja, lakini kwa kufuata kwa makini kanuni ya kutokuwa na zaidi ya theluthi moja ya waumini kwa pamoja, pamoja na  taratibu zingine za wizara ya afya.

 

  1. Utoaji wa huduma kwenye sehemu za kuuza vileo umesitishwa katika kaunti za Nairobi, Nakuru, Machakos, Kiambu na Kajiado. Migahawa katika kaunti hizo zitatoa huduma ya chakula cha kubeba tu, na ni marufuku kuuza vileo.

 

  1. Shule, pamoja na vyuo vikuu vimefungwa. Hakuna kuhudhuria masomo moja kwa moja hadi itakapotangazwa tena. Hata hivyo, wanafunzi wanaofanya mitihani wanruhusiwa kwendelea nayo kwa sasa.

 

  1. Maafisa na wafanyakazi wote wa mashirika ya kibinafsi na ya serikali wameelekezwa kufanya kazi zao wakiwa nyumbani hadi hapo itakapotangazwa tena, isipokuwa wale ambao ,hawawezi kutoa huduma au kutekeleza majukumu yao wakiwa nyumbani.

 

  1. Hospitali zote zimetakiwa kupunguza idadi ya wageni kwa wagonjwa kuwa mgeni mmoja tu kwa kila mgonjwa.

 

  1. Mikusanyiko yote inayoruhusiwa isiwe na zaidi ya watu 50.
READ ALSO  Kenyan Catholic priest dies in suspected suicide

 

Mazishi yafanywe ndani ya saa 72 za uthibitisho wa kifo, na yahudhuriwe na watu wasiozidi 50.

Ndoa na hafla zingine zinazofanana zisihudhuriwe na zaidi ya watu 30.

 

  1. Wle walio na umri wa zaidi ya 58 watapewa chanjo katika awamu ya kwanza inayoendelea kwa sasa.

 

 

Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Copyright © 2023 Kenya Satellite News Network. All Rights Reserved.